SIMBA YAIFUATA YANGA ZANZIBAR
Kikosi cha Simba leo jioni kinatarajiwa kusafiri kwenda visiwani Zanzibar kupiga kambi ya wiki nzima kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ngao ya jamii unaotarajiwa kuchezwa tarehe 23 Agosti jijini Dar es Salaam.
Watani wa jadi Simba na Yanga ndiyo watakutana katika mechi ya ufunguzi rasmi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018 mchezo ambao unatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na klabu hizo msimu huu kuwa na mabadiliko ya aina yake katika vikosi vyao.
Klabu ya Yanga ilitangaza kupiga kambi kisiwani Pemba kwa wiki moja kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo na Simba nao wameamua kuwafuata watani wao wajadi huko huko Zanzibar nao wakijandaa dhidi ya Yanga na michezo mingine katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 26 mwaka huu.
Post a Comment