Header Ads

SHAMSA ATAMANI KUMFUATA MZEE YUSUF


Staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford.
STAA wa sinema za Kibongo, Shamsa Fordamefunguka kuwa, anatamani kumfuata aliyekuwa staa wa Taarab, Mzee Yusuf kwa kuokoka kwani anahisi siku za kufa zimekaribia.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kuwa, kila kukicha anajikuta anatamani kuokoka na kuacha kila kitu anachokifanya, abaki kusali tu kwani ana hofu sana ya Mungu, lakini hajui ataanzaje, ingawa anajitahidi. “Nimejaribu kusali sala tano kila siku.

Kuna wakati ninasahau lakini kuna siku ninasali zote, ninaamini taratibu nitakuwa kama Mzee Yusuf, ninamuomba sana Mungu,” alisema Shamsa.
STORI: HAMIDA HASSAN, RISASI JUMAMOSI

No comments