ROMA ATUA BONGO KWA KISHINDO AKITOKEA ZIMBABWE (VIDEO)
Staa wa ngoma inayofanya vizuri kwa sasa, Zimbabwe, Ibrahim Mussa ‘Roma’ ametua Bongo akitokea katika ardhi ya Rais Robert Mugabe, Zimbabwe alikokuwa ameweka kambi kwa muda.
ROMA ATUA BONGO
Roma ametua usiku wa kuamkia leo (Jumatano), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na kupokelewa na mashabiki wake pamoja na wasanii wenzake.
“Nimeamua kurejea nchini ili niwe karibu na familia yangu, pia namshukuru sana mke wangu kwa kuitambulisha ngoma yangu kwa Watanzania, na kuniwakilisha kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
“Nimerudi mwenyewe sasa nitatembea katika vyombo mbalimbali vya habari ili niwaeleze Watanzania maana halisi ya ngoma yangu ya Zimbabwe,” alisema Roma Mkatoliki.
NA ISRI MOHAMED/GPL
Post a Comment