RAIS MAGUFULI AMTEUA MKURUGENZI MKUU MPYA WA NHIF
Rais John Magufuli amemteua, Bernard Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Konga umeanza Agosti 9, 2017.
Kabla ya uteuzi huo Konga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Post a Comment