Header Ads

Mahakama yaruhusu mkutano mkuu wa club ya simba kufanyika Agosti 13


 Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba la kutaka kuzuia mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika August 13 mwaka huu.

Hakimu Mkazi amesema haitokua busara kuzuia mkutano huo kwani Agenda za mkutano  hazionyeshi kama kuna agenda ya mabadiliko ya mfumo kama ambavyo wadhamini wanadai.

Pia Mahakama imesema sio busara kuzuia Mkutano kwani tayari baadhi ya wanachama wa Simba wanaoishi mikoani wameshawasili hivyo kuzuia mkutano huo ni kuwatia hasara, lakini pia uongozi wa klabu umeshafanya maandalizi.

Na mwisho kabisa mahakama imesema kwa kuwa mlalamikaji ambae ni Mzee Kilomoni ana haki ya kuhudhuria Mkutano Mkuu ni vema akaenda kwenye mkutano huo akaeleza maoni yake.

No comments