Header Ads

Orodha ya wanaowania tuzo za Uefa hii hapa


Tarehe 24 mwezi huu wa 8 pale mjini Monaco nchini Ufaransa kutakuwa na hafla ya kukabidhi tuzo kwa wale waliofanya vizuri katika michuano ya Champions league na ile ya Europa league na hii leo Uefa imetoa orodha ya wanaowania tuzo hizo.
Tuzo ya mchezaji bora wa Champions League yupo Cristiano Ronaldo ambaye aliisaidi timu yake kuchukua kombe,yupo Paulo Dyabala ambaye aliipeleka Juventus fainali na yupo mfungaji bora wa La Liga Lioneil Messi.
Katika kinyang’anyiro cha kiungo bora wa Champions League majina yaliyojitokeza ni ya kutoka Real Madrid tu kwani yupo Toni Kroos, Luca Modric na yupo mkata umeme wa Real Madrid Casemiro.
Golikipa bora yupo Gianluigi Buffon toka Juventus, vilevile yupo Manuel Neuer toka klabu ya Bayern Munich na mwisho yuko Jan Oblak anayekipiga Athletico Madrid.
Walioko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya mlinzi bora yupo Marcelo kutoka Real Madrid, yupo Sergio Ramos naye mlinzi wa kati wa Real Madrid na yupo Leornado Bonucci aliyehamia Ac Millan hivi karibuni akitokea Juventus.
Lakini katika tuzo za mchezaji bora wa michuano ya Europa, wachezaji wote watatu wanaowania tuzo hiyo wanatokea Manchester United, yupo Paul Pogba, Zlatab Ibrahimovich na yupo Henrikh Mkhitaryan.

No comments