Header Ads

NIYONZIMA: KWA MWENDO HUU, MTAUMIA WENGI


Haruna Niyonzima.

KIUNGO mchezeshaji wa Simba,Haruna Niyonzima, ameweka wazi kuwa kwa staili ambayo wameanza nayo ya kufunga idadi kubwa ya mabao, timu nyingi zitaumia zikikutana na muziki wa ‘Mnyama’.
Niyonzima alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoanza vizuri harakati zake za msimu huu baada ya kuifunga Ruvu Shooting mabao 7-0, kwenye pambano la ligi kuu lililopigwa Uwanja wa Uhuru, juzi Dar.
Kiungo huyo ameliambia Championi Jumatatu kuwa kuanza ligi kwa idadi kubwa ya mabao ni ishara nzuri kwao ambapo inawaweka kwenye njia nzuri ya kuanza harakati za kutwaa ubingwa wa msimu huu.
“Kila mmoja ameona jinsi ambavyo tumepambana na kuifanya timu kuanza vizuri katika ligi, tena kitu kizuri ni kwamba tumeanza kwa idadi kubwa ya mabao.
“Naamini kwamba tukiendelea kwa namna hii, basi hakutakuwa na wa kutuzuia, na hilo tuna asilimia kubwa ya kulitimiza kwa sababu kila mmoja hapa anawaza kuifanikisha timu itwae ubingwa tu,” alisema Niyonzima.
Said Ally na Musa Mateja

No comments