Header Ads

Mayanja kampongeza Juma Luizio baada ya Simba kushinda 7-0

Na Zainabu Rajabu

MARA baada ya Simba SC kupata ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amempa pongezi mchezaji wake Juma Liuzio kwa kazi nzuri aliyoifanya.
Simba imepata ushindi huo katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara uliopigwa Jumamosi August 26, 2017 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mayanja wakati anazungumza na waandishi wa habaru amesema, Liuzio amefanya kazi kubwa sana kwa kucheza kwa akili huku akitoa nafasi kwa Emmanuel Okwi kufunga.
“Mechi zinazokuja pengine inaweza kutokea tumeshinda tatu, nne au tano, kwa sababu baada ya kushinda Ngao ya Jamii imetupa morali sana katika timu yetu,” Mayanja.
“Licha ya kupata ushindi huu mnono lakini nampongeza Liuzio kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kushirikiana na Okwi.”
Mayanja ambaye ni raia wa Uganda, aliwapongeza wachezaji wa Ruvu Shooting kwa mchezo mzuri waliouonesha licha ya kuzidiwa na kukubali kichapo hicho.

No comments