Diamond afafanua sababu ya kuweka picha ya Alikiba ofisini kwake
Msanii wa Muziki Bongo, Diamond Platnumz ametoa sababu ya kuweka picha ya Alikiba katika ofisi yake ya WCB.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ya Eneka, ameimbia Clouds Fm Top 20 kuwa ameweka picha ya kila msanii ambaye ana mchango mkubwa katika kukuza muziki wa Bongo Flava.
“Ile siyo ofisi ya Diamond, Rich Mavoko, Harmonize, siyo ofisi ya Tale, ni ofisi ya muziki wa Bongo Flava ambayo imeweka kuona ni kwa namna gani inaweza kuinua muziki wa Bongo Flava,” amesema na kuongeza.
“Bongo Flava haikuletwa hapa tu pekee yangu na wana WCB lakini kuna wasanii tofauti tofauti wana mchango wao katika muziki wa Bongo Flava, so tumeweka baadhi ambao wanamchango, tulitamani tuweke wengine wengi lakini nafasi isingetosha, tumechagua wachache ambao wana mchango,” amesema.
Ameongeza kuwa watu wanaohoji au kushangaa kitu hicho ni hisia tu na kila mtu anapaswa kuwa na hisia zake lakini haikuwa hivyo kama wanavyofikiria.
Post a Comment