200 WAUAWA KWENYE MAPOROMOKO YA ARDHI, SIERRA LEONE
WATU 200 wameuawa na wengine ambao idadi yao haijafahamika hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi kuikumba Sierra Leone leo Jumatatu, Agosti 14, 2017.
Taarifa zimeeleza kuwa, eneo moja la milima liliporomoka mapema kufuatia mvua kubwa, na kusababisha nyumba nyingi kufukiwa na udongo na mawe yaliyokuwa yakishuka kutoka milimani.
Baadhi ya raia waliokuwa eneo la tukio wameokolewa huku maafa makubwa yakiarifiwa kutokea katika Mji wa Free Town.
Post a Comment