Header Ads

BELLE 9 AFUNGUKA KUWAKACHA MADAIREKTA WABONGO


Mwanamuziki Belle 9.
MWANAMUZIKI anayefanya poa Bongo kwa sasa na Wimbo wa Mfalme, Abednego Damian ‘Belle 9’, amefunguka kuwa kitendo chake cha kufanya video na madairekta wa nyumbani katika baadhi ya kazi zake, si kwamba hakubali uwezo wao bali anahitaji kuchanganya ladha tofautitofauti kutoka kwa madairekta wa nje na nyumbani ili kuzidi kuwapa vitu vizuri mashabiki wake pia.

Belle 9 afunguka

Akichonga na Uwazi Showbiz, Belle alifunguka kuwa video zake nyingi amefanya na madairekta wa Bongo lakini anapoamua kutoka kama alivyofanya kwenye video yake ya sasa ya Wimbo wa Mfalme, aliyofanya na Kelvin Bosco JR, kutoka Kenya si kwamba amewakacha madairekta wa Kibongo.
“Kufanya kazi na madairekta wa nje ni namna ya kuchanganya ladha kwenye kazi zangu ili kuwapa mashabiki vitu vizuri zaidi. Nimefanya nyimbo nyingi na madairekta wa hapa nyumbani na kuna wakati inabidi nitoke na kwenda nje,” alisema Belle 9.

NA: BONIPHACE  NGUMIJE

No comments