Header Ads

USAJILI: Man City yasajili beki hatari wa Spurs


Klabu ya Manchester City imethibitisha kumsaini beki wa kulia wa Tottenham, Kyle Walker kwa mkataba wa miaka mitano.
Mchezaji mpya wa Man City, Kyle Walker aliyesajiliwa kwa dau la pauni milioni 50
City imemsajili mchezaji huyo atakaye valia jezi namba mbili ndani ya kikosi hicho kwa dau la pauni milioni 50.
Mauricio Pochettino anafuraha kuwa sehemu ya kijana, Kyle Walker kabla ya kukiacha rasmi kikosi hicho
Mara baada ya kukamilika kwa usajili huo, Walker mwenye umri wa miaka 27 amesema anafuraha kujiunga na kikosi hicho.
“Kocha, Pep Guardiola ni miongoni mwa walimu wenye heshima kubwa duniani hivyo nina imani ataweza kunisaidia kuinua kipaji changu”. Amesema Kyle Walker.

No comments