Header Ads

Tetesi na usajili wa ligi kuu Epl


Klabu ya Aston Villa imekamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa kati wa timu ya Chelsea John Terry ambaye atakuwa na klabu hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.
Klabu ya West Ham ya nchini Uingereza inajipanga kumrudisha mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez ambaye kwa sasa anacheza Bayern Leverkusen.
Lakini wakati Everton wanajiandaa kuja nchinj Tanzania, mshambuliaji wa klabu hiyo Romelu Lukaku bado anaipasua kichwa Chelsea na Conte yuko tayari kutoa pesa yoyote kumnunua.
Baada ya usajili wa Thomas Lemar kutoka Monaco kwenda Arsenal kuonekana mgumu sasa kocha Arsene Wenger amehamisha nguvu zake kwa Riyad Mahrez.
Klabu ya Everton ambayo iko katika hatua za mwisho mwisho katika maandalizi yake ya safari ya kuja nchini Tanzania inataka kutuma ofa ya €20 kumnunua Olivier Giroud.
Inasemekana mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid James Rodriguez amewaambia Real Madrid kama wanataka kumuuza hataki kuuzwa pengine popote zaidi ya Manchester United.
Jose Mourinho hataacha haramati zake za kumfukuzia Romelu Lukaku hata kama Manchester United watafanikiwa kumsajili Alvaro Morata .

No comments