Header Ads

Simba SC kuanza mazoezini leo – Joseph Omog





Kocha Mkuu wa Simba SC, Mcameroon, Joseph Omog, anatarajia kuanza kibaruachake rasmi hii leo cha kukinoa kikosi cha Simba SC kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi  Kuu Tanzania Bara mara baada ya kutua nchini juzi akitokea kwao Cameroon alipokuwa kwenyemapumziko


Omog, ataanza harakati zake hizo za kukisuka kikosi hicho katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo anaamini amerejea nchini kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anakisuka upya kikosi hicho ili msimu ujao kiweze kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu na ile ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumzia usajili wa timu hiyo, amesema kuwa ni mzuri na wachezaji wote waliosajiliwa mpaka sasa anawajua, hivyo kazi kubwa atakayokuwa nayo ni kuwaunganisha ili waweze kucheza kitimu.
Joseph Omog, anaamini kurudi kwake mapema kutakifanya kikosi hicho kiwe imara zaidi katika michezo yake mbalimbali ukizangatia kuwa kunawachezaji wengi wapya waliyosajiliwa.

No comments