NORWAY YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA DOLA MILIONI 10.5 KUBORESHA ELIMU
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende wakielezana jambo kabla ya
kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya
Sekta ya Mafuta, Jijini Dar es salaam.
SERIKALI
ya Norway imeipatia Tanzania msaada wa Dola Milioni 10.5 za Marekani
kupitia programu ya miaka mitatu ya maboresho ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania, inayotarajiwa kuanza Mwaka Mpya wa Fedha- Julai Mosi mwaka
huu.
Mpango
huo pamoja na uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Program ya Maendeleo ya
Sekta ya Mafuta, umezinduliwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya
Nje wa Norway Borge Brende, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip
Mpango na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt.
Juliana Pallangyo kwa niaba ya Serikali zao.
Dkt.
Mpango ameishukuru Serikali ya Norway kwa msaada huo mkubwa
utakaochangia kuboresha utendajikazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa
kuijengea uwezo zaidi wa kitaalamu, miundombinu na vitendeakazi vingine
vitakavyo changia kuongeza uwezo wa Mamlaka hiyo wa kukusanya mapato ya
Serikali.
Kwa
upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi
Dkt. Juliana Pallangyo amesema kuwa hatua ya Serikali ya Norway
kuendelea kufadhili programu ya pili ya Mpango wa kuendeleza Sekta ya
Mafuta utaiwezesha Serikali kubobea katika masuala ya utaalamu wa
masuala ya sheria na usimamizi wa sekta hiyo.
Nae
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende amesifu utendaji
kazi mahili wa Mhe. Rais Dokta John Pombe Magufuli wa kupambana na
ufisadi na vitendo vya rushwa pamoja na kuimarisha ukusanyaji kodi,
hatua ambayo itaifanya nchi ipige hatua za maendeleo haraka.
Amesema
kuwa hajawahi kuona nchi yoyote duniani ikiendelea bila kuweka nidhamu
na uwajibikaji serikali pamoja na kutokusanya mapato yake ipasavyo na
kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya
tano kufanikisha mipango yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (wa tatu kushoto)
akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka
mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa
awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es
salaam.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango,
Benny Mwaipaja akitoa dondoo na kuwakaribisha Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Waziri wa Mambo ya nje wa Norway
Mhe. Borge Brende muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka
mitatu Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa
awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende akielezea kuhusu kuendelea
kwa ushirikiano wenye tija na Tanzania wakati wa kuzindua rasmi Mpango
wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya
pili ya program ya maendeleo ya Sekta za Mafuta jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana
Pallangyo wakinukuu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Mambo ya
Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (hayupo pichani) wakati wa kuzindua
rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya program ya maendeleo ya Sekta za
Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza
jambo wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program
ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), Waziri
wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (katikati) na Balozi wa
Norway nchini Tanzania Hanne Marie Kaarstad wakimsikiliza Kaimu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo
(hayupo pichani) wakati akielezea umuhimu wa Program ya Maendeleo ya
Sekta za Mafuta, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya maafisa waandamizi wa Serikali na waandishi wa habari wakiwa katika
uzinduzi rasmi wa Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya
Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es Salaam.
Maafisa
waandamizi wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia
ushirikiano wenye lengo la kuboresha uchumi unaofanywa na nchi ya Norway
wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya
Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.(Picha: Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-WFM)
Post a Comment