Header Ads

Nafanya kazi kutokana na maoni ya mashabiki – Stamina


Msanii wa Hip Hip nchini Tanzania, Stamina ameweka wazi kuwa muziki wake anaoufanya mara nyingi anatumia ushauri kutoka kwa mashabiki wake.
Stamina
Stamina amesema zamani alikuwa na utaratibu wa kutoa ngoma kila miezi nane lakini kwa sasa kutokana na maoni ya mashabiki wake ataanza kuachia ngoma kila mwezi na hii ni kutokana kuwa na nyimbo nyingi alizomaliza kurekodi.
Mimi nafanya kazi kutokana na Comments za mashabiki zangu, wao ndiyo kila siku wananiambia mzee unakaa kimya sanabhana  tuachie ngoma lakini pia kipindi nilivyokuwa kimya nilikuwa narekodi mno yaani nina mzigo wa kutosha….Nikaona kwanini ngoma zipotee acha tuzitoe tuu unajua hata wanyamwezi huko Billboard wanaingiza ngoma mbili zote zipo Billboard”,amesema Stamina kwenye mahojiano yake na Times FM.
Hata hivyo, Stamina amesema haoni tabu kuachia ngoma kila mwezi kwani anamzio wa kutosha wa ngoma na anaamini anafanya muziki mzuri.

No comments