Header Ads

Daraja refu zaidi duniani la kuning’inia lafunguliwa nchini Uswizi (+video)


Daraja refu zaidi duniani la kuning’inia lenye urefu wa mita 494 limefunguliwa jana nchini Uswizi katika mji wa Zermatt.
Daraja hilo lijulikalo kwa jina la Europabrucke lenye maana ya Daraja la Ulaya lina mita 85 kutoka ardhini litakuwa ndiyo daraja refu zaidi kujengwa likivunja rekodi ya daraja la Reutte la nchini Austria lenye urefu wa mita 405 na mita 110 kutoka ardhini.
Taarifa kutoka Bodi ya Utalii nchini Uswizi zinasema Daraja hilo lina uzito wa tani 8 na limewekwa kifaa ambacho kinazuia lisiyumbeyumbe huku wakieleza kuwa litachochea ongezeko la watalii nchini humo
Daraja hilo lipo kati ya mji wa Zermatt na Grachen kusini mwa Switzerland na limewekwa baada ya barafu kukwangua miamba iliyokuwa ikitumika kuvuka bonde linalotenganisha miji hiyo kitu ambacho kimefanya watumiaji wakwame kuvuka bonde hilo kwa urahisi .
Tazama muonekano wa Daraja hilo.

No comments