Header Ads

Mourinho achoshwa na mabosi wa united





Meneja wa klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza, Jose Mourinho anahitaji kupatiwa wachezaji wake wapya kabla ya safari ya wiki tatu nchini Marekani , United watalazimika kusubiri vilabu vingine vifanye usajili kabla ya kuruhusu wachezaji wao kuondoka.
Kocha wa klabu ya Manchester United(katikati) akiwa katika mazoezi na timu yake
kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports, kocha wa United anataka kukamilisha dili la straika wa Real Madrid, Alvaro Morata wiki hii huku kikosi cha kwanza cha United kinatarajiwa kuanza mazoezi katika viwanja vya Carrington, jumamosi.
Wawakilishi wa Morata walikutana na uongozi wa Real Madrid jana jumatatu asubuhi kuzungumzia mustakabali wa straika huyo.
Mourinho anataka kuimarisha nafasi nne muhimu kwenye kikosi chake na aliwasilisha kwa mtendaji mkuu wa United Ed Woodward mwishoni mwa msimu uliopita lakini klabu mpaka sasa imefanikiwa kumsajili Victor Lindelof pekee .
Mourinho angependa kupata wachezaji wake wapya kabla ya safari ya wiki tatu nchini Marekani , United watalazimika kusubiri vilabu vingine vifanye usajili kabla ya kuruhusu wachezaji wao kuondoka.
Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko na kukamilika kwa dili hilo kutafungua mlango wa kiungo Nemanja Matic kuondoka klabuni hapo na kuungana na Mourinho Old Trafford.
Huku United wakiwa wanahitaji mshambuliaji mwingine baada ya kumruhusu Zlatan Ibrahimovic kuondoka, na mustakabali wa Wayne Rooney bado upo gizani, na uhamisho wa Morata kutua United pia inategemea na Real kupata straika mpya.
Rooney hatarajiwi kuruhusiwa kuondoka United mpaka pale watakapopata straika mpya , ambapo Everton bado hawajafunga mlango kumrejesha Rooney.
Makubaliano ya Rooney kurejea Goodison Park huenda ikawa kwa mkopo , huku United watalazimika kulipa sehemu ya mshahara wake.

No comments