Header Ads

Kukosa promo na kujitenga mitandaoni kumenipoteza – PNC





Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, PNC amefunguka kuwa kukosa promo kwenye vyombo vya habari pamoja na kujiweka mbali na mitandao ya kijamii ni sababu kubwa zilizompoteza kwenye muziki.
PNC
PNC amesema Vyombo vya Habari vilikuwa mbali nae na hata pindi vilivyomfuata vilikuwa vinamuandika kwa habari za kumchoresha kiasi kwamba ulifikia wakati alikuwa anawadanganya Waandishi wa Habari kuwa yupo nje ya Dar es salaam ili kukwepa mahojiano.
Yaani mimi kilichonipoteza kwenye muziki ni uhaba wa promo kwenye Media yaani kuna kipindi ukisikia stori zangu utasikia zile mbaya tuu lakini nzuri zinaachwa kiasi kwamba nikaanza kuogopa Waandishi wa Habari na Watangazaji kwani nilikuwa naona wananichora tuu“,amesema PNC.
Hata hivyo PNC ameongeza kuwa kuwa mbali na mitandao ya kijamii kumemfanya pia watu wamsahau kwenye game kwani anaamini kuna Wasanii wanaishi karibu na mashabiki wao hata kama hawajatoa ngoma kali kwa kipindi kirefu.
Kingine ni kwamba nilikuwa mbali sana na mashabiki wangu hususani kwenye mitandao ya kijamii kwahiyo wengine wakaanza kunisahau taratibu“,amesema PNC kwenye mahojiano yake na Bongo5.
Kwasasa PNC amewaahidi mashabiki wake kuwa wakae mkao wa kula kwani amepanga kutoa ngoma juu ya ngoma na kesho anatarajia kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘NYOTA’ na anaomba Mashabiki wampokee kwa mikono miwili.

No comments