Header Ads

Hii ni wiki ya Cr7, apiga bao mbili kubwa nje ya uwanja


Sahau kuhusu wiki aliyobeba Champions League, sahau kuhusu wiki ambayo Ronaldo alipewa tuzo ya mwanasoka bora na sahau ile wiki ambayo aliwapa Ureno kombe la mataifa Ulaya pale Ufaransa lakini hii inaweza kuwa kati ya wiki bora sana kwa Ronaldo.
Ndoa inanukia, unajua zile mambo ambazo wadada wote wanafanya zikiwa zimekaribia wengi huanza kusoma vitabu vya jinsi ya kuishi na wanaume na wengine huanza kusoma mambo mengi yahusuyo ndoa.
Sasa shemeji yetu kwa Cristiano Ronaldo bibie Georgina Rodriguez amefanya kitendo ambacho kinaonesha yuko katika siku za ukaribu sana na ndoa na tayari ameanza kufanya mipango kuhusiana na harusi yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Georgina ameanza kufollow kurasa zinazohusiana na mambo ya harusi haswa haswa akifollow madesigner wengi wa masuala ya magauni ya harusi ambao inahisiwa huenda ana mpango wa kuwapa kazi kwa ajili ya gauni lake.
Ndani ya wiki moja tayari Georgina amefollowa madesigner watatu wakubwa wa magauni nchini Hispania ambao ni Pronovias,Herve Moreau na Vick Berrecol ambao ni ishara tosha kwamba Georgina anajipanga kwa ajili ya tukio hilo kubwa.
Mimba, wakati habari za ndoa ya Cr7 zikiendelea kufukuta chini kwa chini kuna hili kubwa lingine limeibuka nalo ni kuhusiana na mwanandinga huyu bora wa dunia kukaribia kupata mtoto wa nne.
Ronaldo wakati akifanya mahijiano na jarida maarufu nchini Hispania la El Mundo aliithibitishia dunia kwamba mtoto wake wa nne yuko njiani na ana furaha sana katika kipindi hichi ukizingatia kwamba mtoto huyo atatoka kwa girlfriend wake wa sasa.
Ronaldo alikuwa akizungumza na El Mundo na wakati wakimuuliza kuhusu furaha aliyonayo kwa mapacha wake walimuuliza kwamba anajisikiaje kuhusu mtoto wake ambaye yuko njiani kuzaliwa(na Georgina) ambapo Ronaldo alijibu “yaah nina furaha sana”
Ikumbukwe kwamba hadi hivi sasa Ronaldo hana mtoto hata mmoja ambaye dunia inamfahamu mama yake, kwani Cr7 Jr hadi sasa dunia haimfahamu mama yake, na mapacha wake pia mama yao hawafahamika hivyo mtoto kutoka kwa Georgina itakuwa kitu speciala sana kwa Cr7 kwa sasa.

No comments