Header Ads

Everton wamefungwa 6-0 na Wanafunzi wa Shule ya Msingi


Baadhi ya wachezaji wa Evarton wamefungwa magoli 6-0 wakati wanacheza mchezo maalum wa mpira mpira wa miguu dhidi ya wanafunzi wenye ulemavu wa macho wa Shule ya Msingi  Uhuru Mchanganyiko, Kariakoo, Dar es Salaam.
Wachezaji hao walikuwa ni Leighton  Baines, Idrissa, Gueye, Ademola  Lookman na Yannick Bolasie walifunikwa nyuso zao kwa vitambaa maalumu kisha wakacheza soka na watoto wenye ulemavu wa macho ikiwa ni sehemu ya kujionea ugumu wanaoupata watoto hao kwenye maisha yao ya kila siku.
Mbali na kucheza soka na watoto, pia waliwatembelea walisalimiana na watoto mbalimbali wenye ulemavu wa kusikia, walemavu wa akili pamoja na walemavu wa viungo ikiwa ni sehemu yao ya ziara iliyoandaliwa na serikali ya Uingereza kupitia Wizara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) pamoja na shirika lisilo la kiserikali la kuwasaidia walemavu wasioona na wasiosikia, Sense International.
Mchezaji wa Everton Yannick Bolasie amesema ili mchezaji afanikiwe katika soka ni lazima awe na juhudi na sio kutegemea kipaji pekee.
“Ili mchezaji afanikiwe katika maisha ya soka, kipaji pekee hakitoshi inabidi awe na bidii na kujituma pamoja na nidhamu ili kufikia malengo. Unaweza kuwa na kipaji halkafu unalala ndani, inabidi uoneshe juhudi katika kile unachokifanya,”- Yannick Bolasie.
Everton ipo Tanzania kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ambao ni washindi wa SportPesa Super Cup mashindano ambayo yalishirikisha vilabu nane vya Kenya na Tanzania.

No comments