Header Ads

Emmanuel Okwi atua mazoezini rasmi


Mshambuliaji wa Simba SC na timu ya taifa ya Uganda (The Cranes), Emmanuel Okwi ametua katika kambi ya klabu hiyo iliyopo nchini Afrika Kusini na leo asubuhi ameanza mazoezi.
Okwi amejiunga na wachezaji wenzake katika mazoezi huko Johannesburg nchini Afrika Kusini ambapo timu hiyo ikijiandaa na tamasha lao kubwa la kila mwaka la Simba Day siku ya tarehe 08/08/2017 linalo enda sambamba na utambulisho wa jezi zao mpya, wachezaji waliyosajiliwa pamoja na mechi ya kimataifa.
Kocha Mkuu wa Simba  Mcameroon, Joseph Omog  anaamini kuwa kambi hiyo itawapa nafasi ya kujiandaa vizuri kwa kuwa wapo katika mazingira tulivu.

No comments