Header Ads

USAJILI: Yanga SC yamaliza hasira kwa Mbeya City, yatoka na kiungo tegemezi


                                         Mchezaji wa Mbeya City FC, Raphael Daud
Kiungo nyota wa Mbeya City FC, Raphael Daud amethibitisha kufikia makubaliano ya kusaini mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa Ligi kuu soka Tanzania Bara, klabu ya Yanga SC.

“Nipo katika hatua ya mwisho ya kusajiliwa, nadhani bado na msubiri Kaka angu na wakili wakifika huku kilichobaki ni kusaini hakuna kitu kingine.
“Ndoto yangu ilikuwa nikuchezea Simba au Yanga hivyo ukiangalia ni vilabu vikubwa ambavyo na vinakupa nafasi ya kutoka kwenda kucheza nje ya nchi” amesema Raphael Daudi kupitia kipindi cha Mshikemshike Viwanjani kinachorushwa na Azam TV,.

No comments