Header Ads

TFDA wazungumza kuhusu Mchele wa plastiki


Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeanza kufuatilia madai kuhusu huzalishwa na kutumika kwa mchele wa plastiki nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa (TFDA), Hiiti Sillo, alisema mara baada ya kupata taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii mamlaka hiyo iliunda timu kwa ajili ya uchunguzi.
“Mchele ambao upo na ambao TFDA tunautambua ni wa Basmati ambao huitwa Sunrice. Huu wa kutengenezwa kwa plastiki tunaendelea kufuatilia kama taarifa hizo ni za kweli au la,” alisema Sillo.
“Tayari nimeshatoa maelekezo kwenye kanda zetu za TFDA zikiwamo Mwanza, Arusha, Mbeya kuanza kufuatilia na ninavyozungumza ni kwamba ukaguzi unaendelea. Kama taarifa hizi ni za kweli tunamwomba huyu aliyetuma ‘clip’ (picha) hii kwenye mitandao ya kijamii ajitokeze ili atusaidie ni wapi alikula mchele huu maana clip inaonyesha mkono tu,” aliongeza.
Baada ya picha hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikielezea mchele huo kutumiwa na mamalishe kariakoo jijini Dar es Salaam, kumezua taharuki na gumzo kwa wakazi wa Dar es Salaam ambao asilimia kubwa hula hasa kwa mama lishe.

No comments