Perez raisi tena Real Madrid hadi 2021.
Florentino Perez ataendelea kuwa Rais wa Real Madrid mpaka mwaka 2021 baada ya kutojitokeza mpinzani kabla ya siku ya mwisho ambayo ilikuwa jana jumapili.
Perez alianza utawala wake wa pili mwaka 2009 na ameshuhudia mataji matatu ya UEFA katika kipindi cha miaka minne.
Perez,70 hakupata mpinzani kwenye kugombea wadhifa huo tangu klabu hiyo ilipobadilisha sifa ya kugombea kiti hiko mwaka 2012.
Mabadiliko hayo yanamaanisha kwamba mgombea yoyote anatakiwa kuwa mwanachama wa klabu hiyo kwa miaka isiyopungua 20 ukilinganisha na sifa ya zamani ambayo ilikuwa miaka 10 na awe na kiasi cha fedha binafsi kwenye benki ya Hispania kisichopungua pauni milioni 67.
Kipengele hiko kilifanya kutokuwepo kwa mpinzani yoyote mwaka 2013 na safari hii hakuna aliyejitokeza katika kipindi cha siku 10 tangu mchakato wa uchaguzi ulipoanza Juni 8 na hivyo kumuachia njia nyeupe Perez kuwa Rais kwa mara ya tatu mfululizo na Mara tano kwa ujumla.
Perez kwa mara ya kwanza alikuwa raisi wa Madrid kati mwaka 2000 na 2006 na akamnunua Luis Figo, David Beckham na Ronaldo De Lima na baadae akapewa tena uraisi katika uchaguzi wa mwaka 2009.
Katika kipindi cha mwaka 2009 Perez alipopewa Madrid alifanikiwa kuwanunua Benzema,Cr7,Gareth Bale na Ricardo Kaka ma sasa watu wamsubiri kuona ni nani watanunuliwa baada ya Perez kupewa tena timuu
Post a Comment