Header Ads

Stars dhidi ya Lesotho, Uganda na Cape Verde AFCON leo






Wakati timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inajiweka sawa kujiwinda na mchezo wao dhidi ya Lesotho katika kutafuta tiketi ya kuwania kufuzu michuano ya kombe la Mataifa  ya Afrika (AFCON) mwaka 2019. Mwalimu wa kikosi hiko Salum Mayanga amesema kuwa vijana wake wapo tayari kwa mchezo huo.
“Vijana wangu wapo vizuri, tumejipanga kushinda leo, tunaomba watanzania waje kwa wingi kesho Chamazi kuipa sapoti timu” amesema Salum Mayanga.

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga
Mchezo wa Taifa Stars  dhidi ya timu ya taifa ya Lesotho utachezwa majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Azam Complex.

Mchezo mwingine wa kundi L, utazikutanisha timu ya taifa ya Uganda dhidi ya  Cape Verde  ‘Blue Sharks’ katika uwanja wa Estadio Nacional de Cabo Verde.

Timu ya taifa ya Uganda ikicheza na Senegali  mchezo wa kirafiki
Katika maandalizi ya kuelekea mchezo wao na Cape Verde ‘Blue Sharks’, Uganda Cranes  ilitoka suluhu katika michezo yake miwili ya kirafiki dhidi ya Ethiopia pamoja na Senegal.
Picha wachezaji wa Taifa Stars wakiwa katika mazoezi jana usiku

Michezo itakayo chezwa siku ya leo ya Jumamosi, kufuzu michuano ya kombe la Mataifa  ya Afrika (AFCON) mwaka 2019

No comments