Simba Sc Yasajili Wawili Kutoka Mwanza..Kaburu Adai Anamajina Mengine Sita Makubwa Yatasaini Simba Hivi Karibuni..!!
Klabu ya Simba SC imeanza kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa
Kombe la Shirikisho la Afrika, baada ya jana kukamilisha usajili wa
walinzi wawili kutoka jijini Mwanza.
Simba imevuta beki wa kushoto, Jamal Mwambeleko kutoka Mbao FC na beki
wa kati Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans ambao wote wametokea jijini
Mwanza
Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’
amesema kwamba, Mlipili amesaini miaka mitatu na Mwambeleko amesaini
miaka miwili adai mchezaji Mlipili anatua kwa mara ya kwanza kabisa
Simba SC, wakati Mwambeleko yeye ni kama anarudi nyumbani sababu amewahi
kuchezea timu ya vijana ya Wekundu hao wa Msimbazi.
Mbali na hilo Kaburu baada ya kukamilisha usajili huo amesema mashabiki
na wapenzi wa Simba wakae mkao wa kula kwa taarifa za kuvutia zaidi
kuhusu usajili wa timu yao hiyo ambao unaendelea sasa.
“Kwa ujumla nina wachezaji sita ambao wamekwishakamilisha usajili wao
hapa Simba, lakini nitakuwa nachomoa mmoja mmoja namtambulisha”
Alijinasibu Kaburu

Post a Comment