PICHA 7: Nyumba 3 zinazotajwa kuwa za ajabu zinaoelea kwenye maji
Leo June 19, 2017 nimekusogezea nyumba tatu zinazoelea kwenye maji ambazo ni maalumu kwa ajili ya mapumziko.
Floating Summer House
Nyumba hii ina ghorofa mbili ambayo inapatikana Canada kwenye Ziwa Huron. Nyumba hii hutumika kama makazi ya majira ya joto kwa wapenzi wenye asili ya Cincinnati. Ilimalika ujenzi wake mwaka 2008 ikiwa ni moja ya projects za mwanzo za MOS Architects
Belgrade apartments
Hizi ni hostel na apartments ambazo zinaitwa ArkaBarka zipo katika ukingo wa Mto Danube, Belgrade. Katika jengo hili ambalo huelea kwenye maji lina mambo mengi ya anasa vikiwemo sauna na bar. Zimejengwa kwa kiwango cha hali ya juu ambapo vyumba vyake vinaanzia euro 25.50 na bei zote hujumuisha breakfast na WiFi.
Maldives floating house
Maldives Floating House ilibuniwa na msanifu wa majengo wa Singapore anayeitwa Dymitr Malcew. Kwa mujibu wake ni kuwa alitaka kutengeneza kitu ambacho kitawaruhusu watu kuukubali uhuru na asili. Nyumba ina vyumba viwili vya kulala, vyoo viwili, chumba cha kupumzika na jiko. Nyumba hii ina uwezo wa kusogea kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Post a Comment