Header Ads

Moni Centrozone kuja na lebo


Msanii wa muziki wa hip hop, Moni Centrozone amedai yupo mbioni kuja na lebo ‘Majengo Sokoni’ kwa ajili ya kuwasaidia wasanii wachanga.

Rapper huyo ameeleza kuwa kazi za wasanii hao zitakuwa chini ya usimamizi wa Tongwe Records na kuna baadhi wameshaanza nao.
“Tumelenga kuwanyanyua wasanii ambao wengi wao walikuwa wanahitaji niwasaidie, kwa hiyo nimeandaa project hiyo na mambo mengine yatakuwa chini ya Tongwe Rocords kuhusu kuwasaidia wasanii wao,” ameiambia Twenzetu ya Times FM.
“Tutakua na utaratibu wa kufanya kazi kwa sababu wenyewe tunaangalia na kuchuja kwa kuangalia nani anafanya kazi bora, vile vile tunakaribisha watu kutuma kazi zao, kuna email ambayo tutaweka watu watume kazi ambazo ni nyimbo tatu na kuendelea ili tujue ameshaanza kufanya kitu fulani na sisi tunaweza kumuendelezaje,” amesistiza.

No comments