Mnyama ‘Simba’ auawa shamba la bibi: Nakuru,Gor Mahia zatinga nusu fainali ya SportPesa Super Cup
Klabu ya Simba SC Kutoka Tanzania imetolewa kwenye michuano ya kombe la
Sportpesa Super Cup baada ya kugaragaza na Klabu ya Nakuru All Stars
kutoka Kenya kwa magoli 5-4 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya
kutoshana nguvu dakika 90.
Kwa upande mwingine robo fainali ya mchezo wa kwanza wa leo
uliochezwa kati ya Gor Mahia kutoka Kenya na Jang’ombe Boys kutoka
Zanzibar,Gor Mahia imefuzu kutinga nusu fainali ya Sportpesa super Cup
kwa kuichabanga Jang’ombe Boys goli 2-0.Yanga yatinga nusu fainali ya SportPesa Super Cup Kibabe!!Kwa matokeo hayo Klabu ya Nakuru All Stars itaungana na klabu ya Gor Mahia zote kutoka Kenya kucheza nusu fainali ya Kombe la Sportpesa Super Cup siku ya Alhamisi ya Tarehe 8-June wiki hii saa 10:00 jioni kunako dimba la uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Post a Comment