Header Ads

Kigezo cha kumsainisha Darassa record label


Msanii wa Bongo Fleva na hitmaker wa wimbo ‘Muziki’ ameweka bayana kigezo ambacho anaangalia iwapo mtu anamuhitaji kumsainisha katika lebo.
Rapper huyo ameeleza kuwa kwanza linapokuja suala la lebo ni biashara ambayo unapaswa kuridhia na kujua maslai yako wapi.
“Mtu kama mimi huwa sipiganii maslai yangu tu kwa sababu naamini ningekuwa napigania maslai yangu tu ningekuwa na mafanikio makubwa kuliko wasanii wengine wote kwa kitu ambacho nimekipata lakini huwa naangalia na watu wanaonizunguka kwa kuwa sifanyi hivi vitu pekee yangu,” Darassa ameiambia XXL ya Clouds FM na kuongeza
“Kwa hiyo kutoka kwenye lebo moja kwenda nyingine lazima niangalie na watu wanaoniamini, nimetembea nao safari ndefu lazima ni angali na wao watabaki katika nafasi gani kitendo cha mimi kuchukuliwa kwenda kusaini lebo nyingi.”

No comments