Header Ads

Hata kama nikisaini WCB nitaendelea kuwa shabiki wa Alikiba – AT


Msanii AT amedai anaweza kuwa msanii ndani ya lebo ya WCB lakini haimaanishi kuwa ataacha kumshabikia Alikiba.
Muimbaji huyo amesema kama WCB watakubali baadhi ya vitu anavyohitaji basi anaweza kufanya nao kazi.
“Mimi nitafanya kazi hata Alikiba akisema AT njoo tufanye ninakwenda kufanya ninachoangalia utawezeza kufanya hivi, kama ataweza mimi ninaenda. Sio yeye tu, hata Harmorapa kama anaweza kufanya hivyo mimi nafanya kazi,” AT amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Labda mimi nitaanza kumsaliti Alikiba nisiongee naye, nianze kumsnitch kwa sababu Diamond ananisimamia, haiwezekani. Mimi ninafanya kazi kwa misingi ya kwangu mwenyewe, hata akiwa boss wangu atajua anafanya kazi na mtu ambaye hamshabikii, yaani hata kesho (WCB) wanichukue siwezi kumshabikia Diamond,” ameongeza.

No comments