Header Ads

Alichozungumza Ally Mayay na kocha Julio baada ya kuchukua fomu ya Urais wa TFF

Image result for ally mayai
Juni 19, 2017 mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Ally Mayay ‘Tembele’ alifika kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea Urais wa TFF.
Mayay aliwasili kwenye ofisi za TFF akiwa amesindikizwa na wachezaji wenzake wa zamani pamoja na kocha Julio ambao wote kwa pamoja wanamuunga mkono nyota huyo wa zamani soka Bongo.
Baada ya kuchukua fomu, Mayay amesema kuungwa mkono na watu kunampa faraja na kunamsukuma kuelekea kwenye dhamira aliyopanga kuitimiza.
“Kuungwa mkono na watu kama hivi kunatia faraja na kinakusukuma kwa ile dhamira ambayo mmekubaliana kwenda kuitimiza.”

No comments