CUF Lipumba yatambulisha bodi mpya ya wadhamini, yadai kupata
Uongozi
wa CUF, unaotambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini,
umeitambulisha rasmi bodi mpya ya wadhamini baada ya kupata usajili Juni
12, mwaka huu kutoka Wakala wa Ufilisi na Udhamini (Rita).
Kwa
mujibu wa Sheria namba 5 ya mwaka 1992 ya vyama vya siasa, inakitaka
kila chama cha siasa kilichosajiliwa kuwa na bodi ya wadhamini iliyopata
usajili Rita, ambayo itadumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari leo, (Jumatano) Katibu Mkuu wa
Bodi hiyo, Thomas Malima amesema baada ya usajili huo, Baraza Kuu la
Uongozi chini ya Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba liliketi na kufanya
uteuzi wa wajumbe tisa wa bodi hiyo baada ya kujiridhisha bodi
iliyokuwapo imemaliza muda wake.
“Sasa
chama kinarejea katika hali yake na kumaliza migogoro yote, baraza
moja, kamati ya utendaji moja na Bodi ya wadhamini moja, tunatoa onyo
kali na tutamchukulia hatua kali za kinidhamu mwanachama yeyote
atakayesikika akitoa matamko yoyote yanayohusiana na chama
asiyetambuliwa kikatiba,” amesema Malima.
Kadhalika
Malima ametaja maazimio ya kikao cha bodi hiyo mpya kilichoketi Juni
17, mwaka huu na kusema bodi hiyo iliadhimia kufuta kesi zote
zilizofunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini.
Mengine
yaliyoadhimiwa ni kuziandikia benki zote zenye akaunti ya CUF
zifungulie miamala yake na akaunti ya NMB tawi la Temeke iwe akaunti ya
bodi ya wadhamini.
Post a Comment