Ben Pal Akubali Ombi la Mchekeshaji Ebitoke la Kutaka Kumuoa ,Amtaka Waonane Ili "Wajuane Zaidi"..!!!
Baada ya ombi la mchekeshaji anaekuja kwa kasi kutoka Timamu African
Media, Ebitoke la kuweka wazi hisia zake za kimapenzi kwa msanii wa
Bongo Fleva, Ben Pol huku akimtaka amuoe ikibidi, hatimae mkali huyo wa
RnB amemjibu kwa kusema atafurahi wakionana uso kwa uso.
Ben Pol amesema maombi hayo ya mrembo ‘Ebitoke’ aliyaona mitandaoni
tangia jana ila hakuamini kwani alijua ni stori tuu za mitandaoni mpaka
leo baada ya kuona video ikisambaa Instagram ikimuonesha mrembo huyo
akibubujikwa na machozi huku akimtaka amuoe.
“Kweli nimeziona habari mitandaoni tuu tangia jana watu wakiposti lakini
sikuamini siunajua habari za mitandao bro! ila leo pia nimeona video
yake akisisitiza ombi lake lakini bado siamini na nitaamini na
nitafurahi kama tukionana uso kwa uso.”amesema Ben Pol kwenye mahojiano
yake na Bongo5.
Hata hivyo Ben Pol amesema anaheshimu sana hisia za kila mtu na kitendo
cha Ebitoke kutamka hadharani kuwa anavutiwa nae amekiheshimu na
kukichukulia kwa uzito.
“Kwanza niseme tuu naheshimu hisia za kila mtu yeye ni binadamu na ameonesha hisia zake soo naziheshimu sana.“amesema Ben Pol.
Ben Pol ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Tatu’
aliyomshirikisha Darassa, wiki tatu zilizopita alikuwa ni gumzo
mitandaoni baada ya kuposti picha iliyoleta utata mitandaoni.

Post a Comment