Aslay Afunguka Mambo Haya Matatu Ambayo Kamwe Hatayasahu Kuhusu Ya Moto Band..!!!
Msanii wa muziki Aslay anaye tamba na kibao cha ‘Angekuona’ azungumzia
mafanikio aliyoyapata akiwa na Bendi ya Yamoto ikiwa chini ya mkubwa
Fella amesema ni mengi ila haya ni machache na yenye kipaumbele katika
mafanikio yake kimuziki
Kutembea Nchi mbalimbali
“Yamoto bandi tumeweza kutembea sehemu mbalimbali hapa duniani jambo
ambalo ni neema kwa mwanamuziki kwakutengeneza Connection, tumezunguka
marekani,Asia na Hata baadhi ya nchi za afrika kama vile Rwanda na
kwingineko”
2.Kujengewa Nyumba
“Tumejengewa nyumba tukiwa yamoto bandi kila msanii anayumba yake ,hilo
ni jambo kubwa sana kwani kuna baadhi ya watu wanafanyiwa management
lakini hawapati nafasi hiyo binafsi namshukuru sana Mkubwa Fella kwa
kutufanya tuwe na makazi ”
3.Kuwa mimi kama mimi na kujijenga zaidi
“Kwasasa ninamaisha yangu ambayo naweza kupata riziki za hapa napale na
ninaweza kuendesha familia yangu vizuri pasipo na shida na nimefanikiwa
kufungua biashara ndogo ndogo ambazo zinaniingizia kipato cha kila
siku”

Post a Comment