Wenger akubali mkataba wa miaka miwili
Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekubali kuchukua mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo, jambo ambalo litamfanya kocha huyo kusalia The Gunners hadi mwishoni mwa mwaka 2019.
Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke, walikutana hapo jana kuamua mustakabali wa meneja huyo, na kisha uamuzi wao ukawasilishwa katika mkutano wa bodi hii leo.
Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke, walikutana hapo jana kuamua mustakabali wa meneja huyo, na kisha uamuzi wao ukawasilishwa katika mkutano wa bodi hii leo.
Maamuzi yaliyo fikiwa katika kikao hicho cha bodi ya Arsenal yata tangazwa rasmi siku ya Jumatano hii, mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
The Gunners walimaliza katika msimamo wa Ligi kwa kushika nafasi ya tano ikiwa ni mara ya kwanza kumaliza nje ya nne bora tangu Wenger alipo chukua mikoba ya kuinoa Arsenal mwaka 1996.
Wenger aliongoza Gunners kushinda mataji matatu ya Ligi ya Uingereza pamoja na vikombe vinne vya FA misimu yake tisa ya kwanza.
Wenger aliongoza Gunners kushinda mataji matatu ya Ligi ya Uingereza pamoja na vikombe vinne vya FA misimu yake tisa ya kwanza.
Mfaransa huyo aliweka historia kubwa mwaka 2003-04, baada ya kuwa Kocha wa kwanza kumaliza ligi bila ya kufungwa na timu yoyote tangu ilipo wahi kutokea hivyo miaka ya 1888 – 89
Toka mwaka 2005 walipo shinda taji la kombe la FA walikaa miaka tisa ikiwa ni sawa na siku 3,283 bila ya kuchukua taji lolote kabla ya kushinda taji lingine, mwaka 2014 ambapo waliilaza klabu ya Hull City katika mchezo wa fainali wa kombe la FA kisha kushinda tena mwaka uliofuata.

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakimtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 67 ajiuzulu, hasa baada ya matokeo mabaya msimu huu. Shutuma zaidi zilitolewa baada ya kufungwa jumla ya mabao 10-2 na klabu ya Bayern Munich katika hatua ya 16 bora ya klabu bingwa barani ulaya.
Post a Comment