Header Ads

Tetesi za Ujauzito wa Mchumba Ronaldo Gumzo


Madrid, Hispania. Tetesi za ujauzito wa mchumba wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez zimezidi kushika kasi baada ya mrembo huyo kuweka picha Instagram akiwa na daktari.

Georgina Rodriguez alituma picha hiyo katika mtandao wake wa Instagram akiwa na daktari siku chache baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa Ronaldo anategemea kupata mtoto mwingine.

Tetesi hizo zilianza baada ya nyota huyo wa Real Madrid kutuma picha yake katika Instagram akiwa ameweka mkono wake tumboni mwa mchumba wake huyo mwenye miaka 22.

Hata hivyo tetesi hizo zilipigwa na mama yake Ronaldo akisema mwanaye hategemei kupata mtoto wa pili kwa sasa.

No comments