TPDC yawataka wananchi kupuuza taarifa zinazosambaa juu ya kufungwa kwa kiwanda cha saruji cha Dangote
Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanania (TPDC) linawataka Wananchi kupuuza
taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba, kiwanda cha
saruji cha Dangote mkoani Mtwara kimefungwa kutokana na Sababu
mbalimbali ikiwemo, kushindwa kwa makubaliano ya mauzo ya gesi asilia
baina ya kiwanda cha Dangote na TPDC.
TPDC
inawataarifu wananchi kwamba, imetimiza makubaliano yote ikiwemo mauzo
ya gesi asilia pamoja na ujenzi wa mitambo ya kusafirishia gesi asilia
hadi kwenye mitambo ya kuzalisha umeme ya kiwanda cha Dangote, tangu
2017.
Aidha taarifa inayosambazwa katika mitando ya kijamii ya mwaka 2016 imepitwa na wakati
Hivi
sasa kiwanda cha saruji cha Dangote kinaendela na zoezi la usimikaji wa
mitambo yake ya kuzalisha umeme kwa gesi asilia. Kazi hii inatarajiwa
kukamilika mwezi ujao(Aprili 2018)
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
Post a Comment