Header Ads

Picha: Wenger azungumza kwa kina na Giroud wakati wa mazoezi yake ya mwisho

Mchezaji, Olivier Giroud ameonekana kuwa katika mazungumzo mazito na kocha wake Arsenal Wenger  wakati wa mazoezi ya mwisho kabla ya kujiunga na Chelsea kwa dau la paundi milioni 35.


Mchezaji huyo rai wa Ufaransa akionekana vema kama sehemu ya kikosi kitakacho ingia uwanjani hapo kesho siku ya Jumanne kuvaana na Swansea City mchezo wa ligi kuu ya England.



iroud atalazimika kuondoka Emirates endapo Arsenal itakamilisha usajili utakao weka rekodi ndani ya klabu hiyo wa kumnasa mchezaji wa Borussia Dortmund straika, Pierre-Emerick Aubameyang.
Wakati wa mazoezi hayo Giroud ameonekana kuwa mwenye furaha na amani akiwa na kocha wake Wenger huku wakifanyiana maskhara ya hapa na pale.
Arsenal wanafurahia ujio wa Aubameyang kutoka Dortmund ambapo watagharimika kutoa paundi milioni 55.4 huku wakitarajia kunyakuwa paundi milioni 35 juu ya uhamisho wa Giroud kwenda Chelsea.

No comments