Header Ads

Gyan wa Simba, Victor Moses wa Chelsea tofauti na Kichuya wa Morogoro




















Binadamu ameumbwa ili aweze kupambana na mazingira yake, Mwenyezi Mungu amempa uwezo wa kujiongeza ili aweze kuishi vema, kuna baadhi ya watu wakipata changamoto ndogo tu huanza kuonesha hisia mbaya mbele za watu hata kuchukizwa na kila atendewalo, katika soka la Afrika kuna baadhi ya mataifa yamekuwa na mafanikio makubwa kiasi yanaweza kushiriki michuano mbali mbali ulimwenguni. (Kichuya unanielewa?)
Hii inatokana na uchu wa wachezaji wake walionao, nchi za Afrika Magharibi zimekuwa vinara katika kutoa wachezaji wengi waliotapakaa katika ligi zote kubwa ulimwenguni, huko kote wanatafuta riziki, kiasi cha taifa kuwa na wigo mpana wa wachezaji, Afrika Magharibi nchi za Nigeria na Ghana huwenda zikawa mfano bora kwa vijana wake kutokata tamaa na kuchangamkia fursa ya soka popote. (Kichuya umeelewa?)
Hali hii tofauti na nchi za Afrika Mashariki, wachezaji wengi wa nchi hizi wamekuwa watu wa kubweteka, hawajitumi, wanalewa sifa huibuka na hupotea kabisa, yupo wapi Said Bahanuzi, Abdulhalim Humoud, hawa ni mfano tu wa wale waliokuja kwa mbwembwe lakini kwa sasa hawajulikaniki walipo. (Kichuya unanipata vizuri?)
Pia wapo mmoja mmoja ambao wanajitahidi kuwa na sifa za kiafrika Magharibi, kama vile Mbwana Samatta, Simon msuva, Thomas Ulimwengu, Abdi Banda na Elias Maguli kwa mbali, hawa ndio wachezaji wachache katika mamia ya wachezaji wanaopambana na maisha. Mungu awazidishie katika Kutafuta bila kuchoka. (Shiza unawaona hawa?)
Bila shaka hakuna asiyemjua Victor Moses wa Nigeria na Chelsea, huyu ni mzaliwa wa Nigeria katika jiji la Lagos, huyu alikua winga machachari kwa vilabu mbali mbali kama vile Crystal Palace, Wigan, Westbrom, Liverpool huko kote alikua winga, alijituma mno licha ya kutolewa kwa mkopo mara kadhaa, hakukata tamaa, ujio wa Antonio Conte Chelsea umembadilisha kutoka winga mpaka mlinzi wa kulia, hajawai kuwa bora kama alivyokua sasa akicheza nafasi hiyo.
Mfumo mpya wa Cattenacio 3-4-3 wa Antonio Conte unamfanya Victor Moses awe bora na anamsikiliza mwalimu kwa kila jambo, kwasasa Anategemewa na kikosi cha Nigeria kuwabeba katika fainali za kombe la Dunia mwaka huu. (Shiza unamjua Moses?)
Moses ana mchezaji mwenzake ambaye wanafanana sana tabia na akili, huyu ni Nicholus Gyan wa pale Simba (wekundu wa msimbazi), huyu alikua Mfungaji Bora huko Ghana katika Club yake ya Dwarf FC inayoshiriki ligi kuu Ghana, Simba ikamnunua ili kutatua tatizo lao la Ufungaji, Lakini amekua hapati nafasi sana kama ilivyo kuwa kwa Victor Moses awali pale Chelsea, ujio wa Masud Djuma na mfumo ule ule kama wa Victor Moses pale Chelsea, Gyan wamekua hatari akiwa kama mlinzi wa kulia.
Amebadilishiwa majukumu kutoka mshambuliaji mpaka mlinzi wa kulia, na ameingia kwenye kikosi bora cha Mapinduzi akiwa kama mlinzi wa kulia. Sababu kubwa ni tabia za wachezaji wa Magharibi hufanya jambo lolote, Gyan na Victor Moses wamezaliwa nchi jirani kutoka Lagos mpaka Accra kwa ndege zinahitajika kilometa 456 tu, ndio maana wanafanana tabia.
Kutoka Accra kwa Gyan mpaka Dar es Salaam ni umbali wa kilometa 4245, hapa Gyan anaanzia wapi kuringa? Kutoka Lagos kwa Moses mpaka London ni bkilometa 5020 hapa Moses anaanzia wapi kudeka? Hawa wanatafuta maisha bila kuchoka. (Shiza, Morogoro mpaka Dar kilometa ngapi vile?) Utanikumbusha.
Shiza Kichuya ni miongoni mwa wachezaji maridadi mwenye uwezo mzuri, magazeti ya Bongo yanamwandika sana kuliko Magazeti ya London yanavyomwandika Victor Moses. Masikini Gyan nani atakuandika? Wewe wakuja tu cheza soka na usiombe kuandikwa.
Mfumo alioutumia kocha wa Simba kule Zanzibar ndio ule unaotumiwa na Antonio Conte pale Chelsea, 3-4-3 au 3-5-2 huu hucheza kwa majukumu zaidi kuliko namba, Shiza Kichuya unaonekana Kumchukiza sana, tangu mchezo wa Ndanda kule Mtwara.
Haonekani kua na furaha, kwakuwa mfumo unafanya akae mbali na goli, na yeye anandoto za kuwa mfungaji bora msimu huu, hivyo ndoto zake zinaelekea kukatika, endapo Masud Djuma ataendelea kumfanya awe mbali na goli. Mchezo wa Mapinduzi Cup dhidi ya URA Kichuya alichezeshwa kama mshambuliaji lakini hapo hakufanya kitu chochote alikua mtalii tu, hali iliyopelekea kufanyiwa madiliko, baada ya mabadiriko yale Shiza Kichuya alikataa kukaa kwenye benchi la timu na kwenda kukaa kwa mashaki huku akionekana kuchukizwa na hali ile!
Huyo ndio Shiza kichuya mtoto kutoka Morogoro mji kasoro bahari na klabu haionekani kama ina mpango wa kumuadhibu maana amefanya utovu wa nidhamu.
Kichuya hafurahii mfumo wa kocha, hivyo anaringa, anadeka kujaribu kuonesha hisia zake kwa vitendo mbele ya mashabiki pale Amani. Kipindi Shiza anagomea benchi, Nicholas Gyan mshambuliaji wa zamani yupo ndani anakipiga kisawasawa kama mlinzi wa kulia, amekubali na anapambana, atamringia nani? Hawezi kutolewa akagomea benchi atarudishwa kwao mapema sana. (Shiza muangalie mwenzako).
Gyan na Victor Moses wakupe funzo kwako na kwa wachezaji wengine wa kitanzania, chezeni nafasi yoyote ambayo utapewa, hakuna kuchagua nafasi, kwa namna hiyo kuja kufanikiwa litakua suala gumu, Victor Moses ameshafnikiwa, Gyan amefanikiwa kuwepo kikosi cha kwanza tu, lakini kwakua amelipata hilo ataanza kutafuta na m

No comments