Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa apandishwa kizimbani na TAKUKURU kwa makosa mawili
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma imemfikisha
mahakamani aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM),
Sadifa Juma Khamis.
Sadifa
ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar amefikishwa leo Jumatatu
Desemba 11,2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwa makosa
mawili.
Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga alisema jana Jumapili Desemba 10,2017 kuwa Sadifa angefikishwa mahakamani leo.
Alisema
kiongozi huyo alikamatwa nyumbani kwake akituhumiwa kwa kuwapa soda
wajumbe wa UVCCM kutoka Mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume cha
maadili.
Kuhanga akithibitisha kukamatwa kwa Sadifa alisema alikamatwa Jumamosi Desemba 9,2017.
Post a Comment