Miili ya askari waliouawa DRC kurejeshwa leo
Miili
ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inarejeshwa nchini leo.
Taarifa
ya ofisi ya habari ya JWTZ imesema miili ya askari hao itawasili nchini
leo Jumatatu Desemba 11,2017 saa kumi na mbili jioni katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Awali,
akizungumzia na waandishi wa habari jana Jumapili Desemba 10, 2017
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema miili ya
askari hao ingerejeshwa nchini kati ya Jumanne Desemba 12, au Jumatano
Desemba 13,2017 kwa ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa
(UN).
Mwakibolwa
alisema askari hao walivamiwa kambini na waasi wa ADF na mapigano
yalidumu kwa takriban saa 13. Alisema askari 14 wa JWTZ waliuawa, 44
wamejeruhiwa na wengine wawili hawajulikani walipo.
Alisema
tukio hilo lililotokea Desemba 7,2017 katika kambi ndogo iliyopo katika
daraja la Mto Simulike, kaskazini mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo
la Kivu nchini DRC.
Post a Comment