Header Ads

Singida United yaikaba koo Yanga


Ushindi wa goli 1-0 ilioupata timu ya Singida United dhidi ya Lipuli unaifanya timu hiyo ya mkoani Singida kufikisha pointi 17 sawa na Yanga pamoja na Mtibwa Sugar.
Licha ya kufungana pointi na timu hilo (Yanga na Mtibwa) Singida United ipo nafasi ya tano kutokana na wastani wa magoli. Tayari timu hiyo imeshacheza mechi 10 za VPL sawa na Lipuli huku vilabu vingine vikiwa vinataraji kucheza michezo ya mzunguko wa 10 leo Jumamosi na kesho Jumapili.
Singida United imepata ushindi wake wa kwanza kwenye uwanj wa nyumbani (Namfua) tangu imepanda kucheza ligi kuu msimu huu, awali timu hiyo ilikuwa ikiutumia uwanja wa Jamhuri Dodoma wakiwa wamepisha ukarabati wa uwanja wa Namfua. Mechi yao ya kwanza kucheza uwanja huo msimu huu ilikuwa dhidi ya Yanga ambapo ilimalizika bila timu hizo kufungana.
Kikosi cha Hans van Pluijm kimepata ushindi wa kwanza baada ya kutoka sare katika mechi tano mfulizo zilizopita. Ushindi huo ni wa nne katika mechi 10 ambazo tayari wamecheza. Singida imepoteza mechi moja tu msimu huu ambapo ilifungwa 2-1 na Mwadui kwenye mechi yao ya kwanza.

No comments