Header Ads

SANAMU YA ADOLF HITLER LA ONDOLEWA KATIKA JUMBA LA MAKUMBUSHO


Picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakitabasamu huku wakijipiga picha na sanamu hiyo katika lango la kambi ya Auschwitz.
Ni wakati jamii ya kimataifa ilipotoa hisia kali kuhusu sanamu hiyo ndiposa makavazi hayo ya De ARCA yalipogundua kwamba yamefanya makosa.
Adolf Hitler kabla hajafa
Makavazi hayo yalipo Jogjakarta, Java yalisema kuwa yalitaka kuwaelimisha watu.
”Hatutaki kuvutia hisia mbaya”, meneja wa operesheni za makavazi hayo Jamie Misbah, aliambia AFP.
Picha katika mitandao ya kijamii zinaonyesha watu kadhaa wakipiga picha na sanamu hiyo ikiwemo vijana wadogo waliovaa nguo za rangi ya machungwa wakipiga saluti ya Nazi.


No comments