Header Ads

Rosa Ree aeleza sababu ya kuwa katika dili kubwa na Diamond

Katika exclusive Interview na Hamisihemedi.com, moja ya maswali aliyoulizwa msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree ni kwanini yeye Diamond ndio wasanii pekee walipata dili la ubalozi wa kinywaji cha Belaire na ukizingatia hana muda mrefu katika game.
“To be honest mimi sijui kwa sababu na mimi nilichaguliwa hivyo hivyo na wao, sikujichagua au nikajipendekeza nikasema na quality fulani ndio wakanichukua kwa hiyo sijui ni quality zipi Belaire waliweza kuangalia na wakasema Rosa Ree anafaa” amesema Rosa Ree.
“Lakini najua kwamba ukiweza kujichukulia kwa uzito fulani na watu wanaweza kukuchukulia kwa uzito huo na kwa thamani hiyo na ukafika katika viwango vikubwa” ameongeza.
Kwa sasa Rosa Ree anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Dow ‘ baada ya kukimbiza na ngoma kama Up In The Air na One Time.

No comments