NAWAL AFUTA TATTOO YA NUH MZIWANDA!
Picha ya Nuh Mziwanda na Nawal, Siku ya Harusi Yao
Ni utamaduni wa mastaa wa Bongo, mara tu wanapoanzisha uhusiano na kukolea kwenye penzi jipya, kujichora tattoo ya jina la mpenzi huyo lakini dhorubainapolipitia penzi lao, hutafuta kila njia za kufuta tattoo hiyo.
Hili limejidhihirisha kwa aliyekuwa mke wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda,anayefahamika kwa jina la Nawal,ambaye kwa sasa amefuta tattooya mzazi mwenziye huyo, baada ya kupigana kibuti na mwanadada huyo kuolewa na mwanaume mwingine anayeitwa Masoud.
Nawal Akiwa na Mume Wake wa Sasa, Masoud
Ubuyu wa Nawal kufuta tattoo ya Nuh aliyokuwa ameichora mkononi mwake, umeanza kumung’unywabaada ya kuzagaa kwa picha inayomuonyesha akiwa ufukwenihuku mkono wake uliokuwa umechorwa jina la ‘Nuh Mziwanda’ ukionekana kufutwa tattoo hiyo na kuchorwa ua.
HISTORIA YA TATTOO HIYO
Nawal alimkuta Nuh akiwa katika kipindi kigumu huku kichwa chake kikiwa na msongo wa mawazo,zilizotokana na kumwagana naQueen wa Bongo Fleva, Shilole,ambapo alikuja kwa kasi ya 4G na kumtuliza mawazo Mbongo Fleva huyo, akaamua kuchora na tattooya jina lake ili kumdhihirishia kuwa anampenda sana.
Nuh Mziwanda na Shilole Kipindi cha Penzi Lao
Penzi lao lilijizolea mashabiki wengi kutokana na jinsi walivyokuwa wamegandana kama ruba, mpaka walipofikia hatua ya kufunga pingu za maisha, wakabarikiwa na mtoto wa kike anayeitwa Anyaghile, kisha ‘Jini Kivuruge’ akaliandama penzi lao na kufanikiwa kuwasambaratisha.
Post a Comment