Header Ads

Kama unatarajia Yanga itapata mteremko kwa Singida Utd, jibu lipo kwa Kaseke


Kuna baadhi ya mashabiki wanadhani Hans van Pluijm (kocha), Nizar Khalfan, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deus Kaseke ambao waliwahi kuhudumu Yanga kabla ya kujiunga na Stand United basi Yanga watapata ushindi kwa mteremko, Kaseke amewaambia mashabiki hao kwamba hakuna kujuana wakati wa kazi.
“Hakuna uhusiano wowote wa sisi kuwahi kucheza Yanga na matokeo ya uwanjani. Kila mtu atakuwa kazini kupigania ushindi kwa timu yake, mimi nitakuwa kazini kuhakikisha timu yangu inapata matokeo kwa hiyo mashabiki waje kwa wingi kutuunga mkono.”
Kucheza dhidi ya Yanga kwa mara ya kwanza tangu aondoke
Kaseke ameanza kwa kusema kwamba, mechi itakuwa ngumu lakini timu yake imejiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo huo utakaokuwa wa tisa kwa timu zote tangu kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu huu (2017/18).
“Mechi itakuwa ngumu kila upande kwa sababu kila timu itakuwa ikihitaji ushindi, sisi tumejiandaa kwa ajili ya kupata usndi kwenye mchezo huo.”
Anacho-miss Kaseke tangu aondoke Yanga
Kama unavyojua, Kaseke aliitumikia Yanga kwa misimu miwili akitokea Mbeya City timu ambayo ilimtambulisha ligi kuu Tanzania bara, akiwa Yanga alipata mafanikio ikiwa ni pamoja na kuchukua ubingwa wa VPL mara mbili, TFF FA Cup, Ngao ya Jamii na  kucheza michuano ya kimataifa (Caf Champions League, Caf Confederation Cap ambako alifanikiwa kucheza hadi hatua ya makundi).
Hamisihemedi.com   imezungumza na Deus Kaseke kutaka kujua ni kitu gani ambacho mchezaji huyu wa zamani wa Mbeya City anaki-miss tangu alivyoondoka Yanga nay eye hakusita kufunguka kwa kusema, washkaji kwake ndio kitu anachoki-miss sana tangu amehama Jangwani.
“Unajua nimekaa Yanga kwa miaka miwili ambapo nilifanikiwa sana, hakuna kitu ninachoki-miss kama washkaji (akimaanisha marafiki) tuliishi pamoja na kufanya mambo mengi sana uwanjani na nje ya uwanja kwa hiyo ni kitu ambacho huwa na-miss sana tangu nimeondoka.”
Pluijm ananifahamu vizuri
“Hans ni kocha mzuri nilikuwa nae Yanga na sasa nipo nae tena Singida United, ananifahamu vizuri na mimi pia nafahamu ni kocha wa aina gani na anataka nifanye nini nikiwa uwanjani kwa hiyo nafurahia kuendelea kucheza chini yake.”
Kesho November 4, 2017 Kaseke atakuna na wachezaji wenzake aliocheza nao akiwa Yanga wakati Singida United itakapokuwa ikicheza dhidi ya timu yake ya zamani kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida mechi ya ligi kuu Tanzania bara. Kaseke aliondoka Yanga baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika.

No comments