Header Ads

KAGERA WANOGEWA NA POINTI TATU, SASA WAZITAKA ZA PRISONS KESHO


MAXIME

Baada ya ushindi wake wa kwanza wakiifunga Ndanda FC, Kagera Sugar wanaonekana kutaka kuendeleza ushindi watakapokutana na Prisons kesho.

Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Prisons kwenye dimba la Kaitaba mjini Bukoba.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Meck Maxime amesema wamejiandaa vizuri na pamoja na kushinda lakini kuna mambo waliyorekebisha.

"Hata kama mmeshinda lakini lazima kuna makosa ambayo mnatakiwa kuyafanyia kazi. Tumefanya hivyo kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Prisons.

"Tunaujua ubora wa Prisons, lakini kikubwa ni kuomba afya njema na uzima ili tutimize tunachotaka kufanya," alisema.

Baada ya ushindi wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Kagera Sugar imesogea hadi katika nafasi ya 12 ikiwa na pointi sita.

Lakini Prisons inaonekana kuwa moja ya timu zilizoanza vizuri  msimu huu kwani baada ya mechi nane, ina pointi 13 katika nafasi ya tano.

No comments