Header Ads

Harry Kane, Winks kuikosa Brazili


Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham, Harry Kane na kiungo Harry Winks watakosa kuitumikia timu ya taifa ya Uingereza katika michezo ijayo dhidi ya Ujerumani na Brazili kufuatia majeraha yanayowakabili.
Kiungo wa klabu ya West Brom, Jake Livermore ameitwa katika kikosi cha timu hiyo ya taifa ili kuziba pengo la Winks huku meneja wa Uingereza, Gareth Southgate akitarajiwa kufanya maamuzi ya kupata mbadala wa Kane.
Wachezaji hao wa Tottenham wanaokabiliwa na majeraha wanaendelea na matibabu na wamefikia maamuzi na kocha Southgate hivyo hawatakuwepo hata katika michezo ya kirafiki inayowakabili timu ya taifa ya Uingereza.

No comments